Mtoto akizaliwa ni mgeni katika dunia kwa hivyo hayajui mambo mengi na hujifunza kila siku iitwapo leo hata uzee wake pengine aweza kosa kuyajua mengine katika siku za uhai wake.
Kujifunza kwake kwatokana na mazingira ambayo wazazi wake wanamchagulia kuishi. Mazingira haya hubadilika kwa sababu kadhaa moja wapo ikiwa ni kuhama kwa familia yake kutoka mahali kwenda mahali pengine.
Mazingira yakuishi yanajumuisha watu na shughuli za watu husika, hali ya hewa na maliasili.
Katika mazingira hayo mtoto huwekwa katika nafasi ya kujigundua ambapo hutambua mambo mbalimbali kuhusu yeye hususani vitu anavyopendelea na asivyopendelea, aina za marafiki, mazingira rafiki, shughuli rafiki na mambo mengi zaidi. Yote ajifunzayo na kuyagundua ndio unaotazamiwa kuwa mtindo wake wa maisha.
Kujitambua ni muhimu katika maisha ya mwanadamu yeyote ili kuepukana na migogoro binafsi katika kufanya maamuzi. Kujitambua kwaongeza idadi ya watu wenye misimamo isiyo pepesuka zaidi tena watu wenye maono na malengo thabiti katika eneo lake.
Mwanzo wa kila badiliko la kijamii ni mtu mmoja aliyedhamiria kuwa chanya na kujigundua yeye mwenyewe kunako mjengea misingi ya maisha ambayo kwa hio hutenda na kuenenda.
Fanya leo, jigundue wapenda nini, na nini hupendi; aina gani ya mziki, aina gani ya maeneo yako unayopendelea kutembelea na kuwepo, na watu wa kuhusiana nao.
JIGUNDUE, JITAMBUE!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni