Jumatano, 19 Oktoba 2016

Ujasiri kama Tembo mbele ya Simba!

Soma na mshirikishe na mwingine!

Upo wakati ambao mtu huchoka, pia upo wakati amabao mtu hukata tamaa, upo wakati ambao tumaini huondoka na ngome ya imani huanguka...

Hizi ni nyakati ambazo kila mwanadamu anapitia na wala si wewe peke yako...

Yanayokusonga si kuwa ni mlima usiofaa kuukwea hata kilele chake na kuufikia upande wa pili, tena si ukuta usioweza kubomolewa na kuufikia upande wa pili, si mto usiofaa kuogelea hata kuifikia ngambo yake, tena si kwamba ni jambo ambalo halijawahi kutokea hapo kale; La Hasha! Lakini yote yamekwisha kuwako japo kwa sasa yaweza kuwa na sura tofauti lakini kusudi na dhamira ndani yake ni ile ile...

Je, umejitazama katika kioo na kuona vile jambo lako lilivyo dogo na la kawaida sana? Unakosea kulitafakari ilihali wapaswa kuona njia ya kupita humo. Badili tu mtazamo wako na kuiona changamoto hio kama jiwe la mchanga wa jangwani ambalo hata kwa kulipuliza kwa hewa ya kinywa chako linasambaa.

Wahitaji si nguvu nyingi ila kidogo tu kulikabili jambo hili fanya kuruhusu sehemu ya wewe ambayo haijawahi onekana kudhihirika katika matendo. Kuwa jasiri kama Tembo mbele ya Simba! Amua leo kutumia mwili wako kwa ukubwa wake na uzito wote na ndovu ulizo nazo kumkabili Simba ambaye mwili wake ni mdogo na silaha zake pekee ni meno na miguu basi hana kingine. Kama Tembo waweza kata mti kwa kutumia mkonga wako na kumpiga Simba ambaye hato stahimili maumivu hayo, sharti akimbie tu! Na tangu hapo Tembo kwa heshima hii atakuwa mfalme wa porini.

Shida yako ni ndogo sana sema sifa yake na muonekano wake pamoja na kujigamba kwake na kutamba kwake kunaifanya iwe ya pekee japo ni ya kawaida. Waweza simama leo na kuvunja rekodi kwa kuishinda hali yako. Simama, pigana na uutwae utukufu ambao kwa huo wewe utakuwa mfalme kwa hali hio; mwenye kuheshimika sana na sifa yako kuenea kila mahali toka nchi hata mbingu!

Tangu hapo utaishi maisha ya ushindi na thamani yake ni kubwa kushinda fedha na vito vya thamani.

Na. Mr. Nathanael Kiyuga.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni